NIJUE KWA UFUPI
Jina langu ni Neligwa Boaz Mugittu, mtoto wa tatu katika familia yenye watoto wanne nikiwa mtoto wa kiume pekee. Baba yangu anaitwa BOAZ MUGITTU ambaye kwa sasa ni marehemu tangu atutoke 26/6/1998 na kubaki na mzazi mmoja tu ambaye ni Mama yangu kipenzi aitwaye ESTHER PHILIP NAPUNIGWA ambao wote ni WANYIRAMBA kwa kabila na Wakristo katika dhehebu la LUTHERAN. Dada yangu wa kwanza anaitwa CHRISTOWELLU ambaye naye ana familia yake anayoishi nayo huko BUNJU, dadangu wa pili anajulikana kama WANONDA aliyetangulia mbele ya haki 21/4/2002 na baada ya wao ndio akatokea kidume chao NELIGWA 8/3/1990 ikiwa ni siku ya Wanawake duniani na wa mwisho ni mdogo wangu aitwaye TYATAWELLU. Nyumbani kwetu ni Ukonga Mombasa na ki elimu ni mwanafunzi katika chuo cha MLIMANI nikichukua Stashahada ya Uandishi wa habari. Elimu ya msingi nilimalizia LUPALAMA 'A' iliyopo Iringa au TOSAMAGANGA HOME BOYS, kidato cha nne nimemalizia KINDOROKO iliyopo MOSHI na kidato cha sita ni TUNDURU iliyopo RUVUMA. Shule nyinginezo nilizosoma ni KURASINI iliyopo Temeke jijini Dar, UKONGA iliyopo Ilala jijini Dar na MWANDU ya Iguguno mkoani Singida zote kwa elimu ya msingi na sekondari ni KALENGA iliyopo Iringa na Juhudi iliyopo Dar. Hiyo ni historia yangu kwa ufupi mengine tutazidi kufahamishana. Nawapenda wote
Friday, August 5, 2011
UZUNGU NOMA
Upendo ni mzuri na muhimu katika maisha yetu lakini tusitumie upendo huo kuwaumiza na kuwatesa wengine wanaotuonyesha upendo huo kwani mtu akikuonyesha heshima mpe heshima yake na hata kama anakudharau mpe heshima yake kwani itamsaidia yule mtu asiyekupa heshima yako kujidharau mwenyewe na kujiona mjinga. Upendo huu nimependa kuuongelea kutokana na maneno ambayo yana uzito ukiyachukulia uzito na mepesi ukiyafanya yawe mepesi nayo si mengine ni maneno ya kiingereza kama vile dear, baby, honey, sweet n.k kwani siku hizi imekuwa kama fasheni watu kuitana na kuandikiana hivyo ambapo si vibaya bali ubaya hutokea mtu anapochukulia tofauti na haina ya mtu aliyemuita kwa mfano watu wa jinsia mbili tofauti ambao ni marafiki mmoja akimuita mwenzake maneno kama hayo akiwa na maana ya kawaida tu ya mpendwa bali yeye huchukulia kama wachumba na kuanza kutangaza kwa wengine na kujisifia hivyo inashusha thamani ya mtu husika kwa wengine na kuonekana ni malaya endapo wanajua kuwa ana mchumba fulani. Kwa hiyo tuwe makini na maneno haya tusipende kuiga na kuwasingizia watu wakati sivyo walivyo. TAFAKARI
Tuesday, June 28, 2011
BABA NAKUKUMBUKA
26/6/1988, Ni siku ambayo haitakuja kusahaulika maisha yangu yote hadi pale na mimi nitakapomfuata mtu aliyenitoka siku kama hiyo tena tuliyekuwa tumelala naye kitanda kimoja lakini kazi ya MUNGU haina makosa namwomba yeye atoaye na atwaaye ailaze roho ya baba yangu mpendwa BOAZ MUGITTU mahala pema peponi Amennnnnnnnnnnnnnnnnnnnnn.
Monday, June 27, 2011
Saturday, April 9, 2011
AIBU SI LAZIMA UTEMBEE MTUPU
Kweli kila mtu ana umuhimu wake duniani awe mfupi au mrefu, mnene au mwembamba, tajiri au maskini na mweupe au mweusi kwa kila kipindi chake cha kuonekana ana thamani mbele ya watu kikifika basi huchanua kama ua. Kipindi cha uchaguzi wananchi huonekana bora sana na hata kuwaona mara nyingi viongozi wao ambao huwa nadra kwa wao kuwaona lakini hufikia kipindi hata hukumbatiana nao kisa tu waweze kupata kura zao kwenye uchaguzi mkuu lakini matokeo yake wakishapata uongozi wananchi hupoteza thamani yao kama awali.
Na kiniumizacho kichwa ni hali niionayo ya kupigana na kutoleana maneno machafu kati ya watu wa nchi moja na wanaojenga nchi moja kwa maslahi ya nchi husika kwa kizazi cha sasa na baadae lakini mwisho wake naona hali mbaya inayoendelea ya kuijenga nchi yetu kwa chuki na kuwepo kwa matabaka baina ya watu ambao Mwalimu Nyerere akuyapendelea na kuyakataza kwa nguvu zote lakini sasa naona yanashamiri kwa chini chini na yakishakomaa itakuwa ni balaa kupindukia katika nchi yetu nzuri yenye vitu vingi tusivyoweza kuvitumia.
Wananchi wanaosema maisha magumu na kuishi kwenye maisha hatarishi hao hao huchukuliwa na kupewa chochote kitu ili mradi wakubwa wapate wakitakacho kwa mgongo wa hao hao wenye hali duni na hii inatisha kwani wanawachukua watu wasio na uelewa wowote wa kisiasa hata kielimu wawe wasikilizaji na kuwapa katiba iliyoandikwa kwa kiingereza wakati hata neno 'Constitution' maskini ya Mungu hawalijui lina maana gani kweli hiki ni kichekesho.
Wanachama wa chama wapo wengi sana ndiyo maana tunashinda kwa kishindo sasa iweje kujaza ukumbi mdogo kama ule mkodi watu tena watoto wasiojua lolote kuhusu mada husika au ndiyo malengo yenu ya kung'ang'ania vitu hata kama vimepitwa na wakati? mabadiliko ni yetu sote na si ya wapinzani tu hivyo kubadilika ni jambo la msingi ili nchi isonge mbele.
Mmoja akaulizwa unasoma akajibu ndiyo nasoma na kuulizwa swali la pili unasoma wapi akajibu kwa kutetemeka aaaaah nimeshamaliza, huo ni mfano tosha kwamba watoto waliojazana ndani hawana uelewa wowote kuhusu jambo la katiba na kusikiliza si vibaya ili waweze kuelewa lakini ubaya ni kuwanunua ili wazibe nafasi za watu wengine ambao wangeuliza maswali yenye mantiki.
Kwa kitendo kile hawajaaibika tu wale watoto bali na Chama husika kilichowanunua watoto wale na kupunguza uaminifu kwa wananchi wake na kuwapa moyo wa kuamini kwamba mambo mengi huwa yanachakachuliwa hivyo nawakumbusha tu wasizidi kukiaibisha chama kwani kuaibika kwa mtu si lazima atembee uchi bali kwa jambo lolote baya.
Imeandikwa na N.B.Mugittu

Friday, April 8, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)